Brazil inahitaji mwanasaikolojia
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari ameagiza mwanasaikolojia kujiunga na kambi ya mazoezi ya timu hiyo kufuatia ushindi mgumu dhidi ya mahasimu wao wakuu Chile.
Wenyeji hao wa kombe la dunia walihitaji muda wa zaida na bahati kuilaza Chile mabao 3-2 jambo lililowaacha wengi wa wachezaji wao akiwemo Neymar wakitoa machozi baada ya mechi hiyo katika uwanja wa Estadio Mineirao.
Neymar alisema "mechi hiyo dhidi ya Chile ilikuwa na umuhimu mkubwa kwetu katika azimio letu la kuffuzu kwa fainali ya mashindano hayo kwa hivyo haikuwa udhaifu ni machozi ya furaha''
Brazil atachuana na Colombia katika robo fainali siku ya ijumaa.
Matumaini ya wenyeji ni kuwa Neymar ataiongoza timu hiyo kunyakua kombe la dunia .
Mshambulizi huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 22 tayari ameifungia timu yake mabao manne.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni