KUMEKUCHA! MPACHIKA MABAO JAMES RODRIGUEZ ATUA REAL MADRID!



James Rodriguez akifanyiwa vipimo mjini Madrid kujiunga na Real Madrid.
Rodriguez wakati akitoka hospitali mjini Madrid baada ya kukamilisha vipimo.…
James Rodriguez akifanyiwa vipimo mjini Madrid kujiunga na Real Madrid.
Rodriguez wakati akitoka hospitali mjini Madrid baada ya kukamilisha vipimo.
Rodriguez akionyesha dole ndani ya Madrid.
MPACHIKA mabao wa Kombe la Dunia 2014, Mcolombia, James Rodriguez, ametua katika klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania kwa dau la pauni milioni 60.
Staa huyo amesaini mkataba wa miaka sita na mabingwa hao wa Klabu Bingwa Barani Ulaya kwa msimu wa 2013/2014.
Rodriguez ambaye tayari amefanyiwa vipimo, anakuwa mchezaji wa nne kwa uhamisho ghali baada ya Gareth Bale aliyesajiliwa kwa pauni milioni 80 sawa na Cristiano Ronaldo kwenda Real Madrid, Luis Suarez uhamisho wa pauni milioni 75 kwenda Barcelona.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA