Neymar alihofia kupooza


Neymar alihofia kupooza
Kocha wa Brazil , Luiz Felipe Scolari, amesema kuwa mshambulizi nyota wa Barcelona ya Uhispania na Brazil Neymar alikumbwa na mshtuko na kuhofia kuwa alikuwa amepooza miguu yake punde baada ya kugongwa uti wa mgongo na kiungo wa Colombia Juan Zúñiga .
Scolari amewaambia wanahabari kuwa alikuwa anasema kuwa miguu yake imekufa ganzi kabla ya kukimbizwa hospitalini mjini Fortaleza ilikupigwa picha ya Xray.
Neymar alihofia kupooza
Daktari wa timu hiyo Rodrigo Lasmar amedhibitisha kuwa Neymar amejeruhi uti wake wa mgongo na kuwa hatoweza kucheza kwa kipindi cha majuma manne hadi 6 yajayo .
Kauli hiyo imemlazimi Scolari kupanga upya safu yake ya mashambulizi ilikufidia pengo aliyoiwacha Mshambulizi huyo machachari.
Neymar akipelekwa hospitalini
Neymar alikimbizwa hospitalini kwa helikopta timu yake ilipokuwa ikiongoza 2-1 dhidi ya Colombia katika mechi ambayo wenyeji hao walijikatia nafasi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani.
Picha za mshambulizi huyo akilia ziliwatamausha mashabiki wake kote duniani .
Neymar alipojeruhiwa na Juan Zuniga
Mashabiki wa Brazil sasa wamesalia na hofu kubwa kutokuwepo kwake huenda ikaifanya selecao kuwa wadhaifu mbele ya Ujerumani timu hizo zitakapokutana sikua ya jumanne.
Scolari amesema kuwa ''Bila shaka tumempoteza mchezaji ambaye anaweza kuleta tofauti kubwa mno katika mechi yeyote ile hususan katika mechi hiyo ya jumanne dhidi ya Ujerumani''

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA