BRAZIL 2014: Gustavo pigo kwa Brazil dhidi ya Colombia leo

Kiungo wa Brazil Luiz Gustavo (kulia) akigombea mpira na Andres Guardado wa Mexico katika hatua za awali za Kombe la Dunia la 2014 kule Fortaleza, Brazil. PICHA | AFP 
KWA UFUPI
Lakini kwa beki ambaye anaweza kuwaweka pamoja wachezaji wote katika safu ya ulinzi na kiungo, Luiz Gustavo anakuwa pigo kubwa kwa mchezo wa leo wa robo fainali dhidi ya Colombia.


Teresopolis, Brazil. Licha ya kuwa Neymar ndiye mchezaji anayetajwa zaidi na kuonekana msaada mkubwa katika kikosi cha Brazil, pia uwepo wa Oscar, Thiago Silva na David Luiz unaonekana kuwa muhimu uwanjani.
Lakini kwa beki ambaye anaweza kuwaweka pamoja wachezaji wote katika safu ya ulinzi na kiungo, Luiz Gustavo anakuwa pigo kubwa kwa mchezo wa leo wa robo fainali dhidi ya Colombia.
“Ningependelea kuacha majukumu yangu kwa wachezaji wenzangu,” alisema mchezaji huyo mwenye miaka 26 aliyesajiliwa na klabu ya Wolfsburg.
“Inanipa furaha moyoni kwamba nimefanya makubwa katika nchi yangu hadi kufikia sasa,” aliongeza kiungo huyo, ambaye hatakuwepo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Brazil, Carlos Alberto Parreira anamtaja mchezaji huyo kama mtu muhimu katika timu akiwa na safu nzuri ya ulinzi duniani.
Katika hatua ya makundi, Luiz Gustavo alifanikiwa kunyang’anya mipira zaidi kuliko mchezaji yeyote wa Brazil na kukimbia kuliko wenzake, akiwaruhusu Daniel Alves na Marcelo kupanda.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA