MICHEPUKO NOMA: ACHANWA NA VYEMBE NA KUTEMBEZWA UMBALI WA MITA 300 BILA NGUO MCHANA KWEUPE MTAA WA MSAMVU B KIHONDA MAGHOROFANI MKOANI MOROGORO
Aliyekatwa nyembe.
MWANAMKE mmoja,
Rehema Juma (21) ambaye ni mke wa mtu, mkazi wa Mtaa wa Msamvu B, Kata
ya Kihonda Maghorofani mkoani Morogoro amechanwa na nyembe mwilini na
baadaye kutembezwa bila nguo mtaani mchana kweupe akituhumiwa kufumwa na
mume wa mtu.Tukio hilo la aina yake ambalo lilivuta umati mkubwa, lilitokea Julai 5, mwaka huu saa 10 jioni katika Mtaa wa Msamvu B.Mashuhuda
wa tukio hilo walipohojiwa na paparazi walidai kuwa kwa muda mrefu,
Zaitun Ally (30) ambaye pia anaishi kwenye mtaa huo alikuwa akimshutumu
Rehema akidai anatembea na mumewe, hivyo akaamua kutega mtego bila
mafanikio.“Zaituni
baada ya kushindwa kuwanasa leo aliamua kumuita Rehema nyumbani kwake
na kudai amewafuma na mumewe hivyo kumchana nyembe baadaye kumvua nguo
na kumtembeza bila nguo mtaani hadi nyumbani kwake umbali wa mita 300
mchana kweupe,” alisema mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa
jina la Ashura Ally.
Maoni
Chapisha Maoni