RAISI KAGAME AWEKA WAZI KUWA YEYE NA TANZANIA DAMU DAMU
Rais Kagame azungumzia uhusiano kati ya Rwanda na Tanzania
Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kwamba Rwanda na Tanzania ni mataifa ndugu na yataendelea kuwa ndugu kwa sababu yanachangia udugu huo.
Rais Paul Kagame ameyasema hayo mjini Kigali kwenye kikao na waandishi wa habari.Nchi za Rwanda na Tanzania zilikabiliwa na wakati mgumu kuanzia mwaka jana kutokana na kutofautiana kuhusu kundi la waasi wa kihutu la FDLR linaloendesha mambo yake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya utawala mjini Kigali.
Mwandishi wetu Sylivanus Kalemera kutoka Kigali ana ripoti zaidi. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni
Maoni
Chapisha Maoni