Ndege Ya Algeria nayo Yapoteza yapotea Angani ikiwa na Abiria 116

0
SHIRIKA la ndege la Taifa la Algeria, limesema limepoteza mawasiliano na moja kati ya ndege zake iliyokuwa ikitoka Burkinafaso kwenda Algiers kupita Sahara.
 
Mawasiliano yalipotea dakika 50 baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji wa Ouagadougou, Burkinafaso shirika hilo limeeleza.
 
Ndege namba AH 5017 ilikuwa na abiria 110 na wafanyakazi sita wa ndege hiyo.
Chanzo cha habari kimeliambia Shirika la Habari la Ufaransa kuwa ndege hiyo haikuwa mbali na mpaka wa Algeria wafanyakazi wa ndege hiyo walipoambiwa wabadili uelekeo kwa kuwa mawasiliano yalikuwa hafifu na kuepuka hatari ya kugongana na ndege nyingine katika njia ya Algiers-Bamako.
Mawasiliano yalipotea baada ya kubadilishwa kwa njia.
plane
 
Ndege namba AH 5017 husafiri kupitia njia ya Ouagadougou-Algiers mara nne kwa wiki, AFP imeripoti.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA