BRAZIL 2014: PIGO LA KARNE: Majonzi, vilio kila kona Brazil
KWA UFUPI
- Mabao ya mshambuliaji Thomas Muller dakika ya11, Toni Kroos ( mawili 24, 26), Klose (23), SamiKhedira (29na Andre Schurrle (69, 79 ), kabla ya Oscar kufunga bao la kufutia machozi dakika 90.
Sao Paulo, Brazil. Vilio, majonzi vilitawala kila ni kona ya Brazil baada ya kupokea kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 7-1kutoka kwa Ujerumani katika nusu fainali ya kwanzajana kwenye Uwanja wa Mineirao.
Ujerumani imeweka rekodi ya kufunga mabao matano ndani ya dakika 30, huku mkongwe Klose akiweka rekodi mpya ya mabao 16 katika Kombe laDunia.
Mabao ya mshambuliaji Thomas Muller dakika ya11, Toni Kroos ( mawili 24, 26), Klose (23), SamiKhedira (29na Andre Schurrle (69, 79 ), kabla ya Oscar kufunga bao la kufutia machozi dakika 90.
Brazil ikicheza bila ya Neymar na nahodha wakeThiago Silva waliuanza mchezo kwa kasi katikadakika 10 za mwanzo, kabla ya Ujerumani kuanzakukisambaratisha kikosi cha Luiz Felipe Scolar.
Thomas Muller alifunga bao lake la tano na la kwanza akiunganisha kona na Kroos kabla ya Miroslav Klose kupachika bao la pili na kuimaliza kabisa Brazil ambao mashabiki wake walianza kuondoka uwanjani.
Kroos alifunga bao tatu na kufunga bao la nne sekunde chache baadaye huku Khedira akifunga bao la tano kwa shuti la umbali wa mita 12.
Schurrle aliingia akitokea benchi na kufunga mabao mawili kabla ya Oscar kuwafuta machozi wenyeji kwa bao lake.
Ujerumani sasa watacheza fainali na mshindi wa mechi ya leo kati ya Argentina au Uholanzi.
Argentina, Uholanzi usipime
Wakichochewa na miaka mingi ya uchungu, Lionel Messi wa Argentina na Arjen Robben wa Uholanzi watashuka kwenye hatua muhimu ya nusu fainali ya Kombe la Dunia kwenye Uwanja wa Corinthians, Sao Paulo kwa lengo la kufuta rekodi hiyo mbaya.
Argentina, ambayo mara ya mwisho kufuzu kwa fainali 1990, wataingia uwanjani kwa lengo la kutoa zawadi kwa gwiji wao wa zamani, Alfredo Di Stefano, aliyefariki dunia Jumatatu akiwa na umri wa miaka 88,
Uholanzi kwa upande wao watakuwa na nia moja ya kufuta rekodi yao mbaya kwenye fainali hizo baada ya mara tatu, mwaka 1974, 1978 na 2010 kuingia fainali na kuondoka mikono mitupu.
Maoni
Chapisha Maoni