MAJANGA! Mke wa Kingwendu Abakwa Live…!
MKE wa Kingwendu ambaye ni muigizaji maarufu wa filamu za vichekesho nchini amefanyiwa kitendo kibaya cha ubakaji na mwanaume aliyefahamika kama Upunguvuku katika pagala moja huko Mbagala Kingugi kwa Kisauti…..
Mke wa Kingwendu anayejulikana zaidi kwa jina la mama Maua, alikutwa na masahibu hayo Alhamisi iliyopita baada ya kuvamiwa na Upunguvuku anayedaiwa kuwa alikuwa amelewa na kuingizwa kwenye jumba ambalo halijasha kujengwa lililopo maeneo ya Kwa Dunga ambapo wapita njia waliwafuma na kuanzisha mtiti…..
Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe amesema kuwa, wakati tukio hilo linatokea, Kingwendu mwenyewe alikuwa safarini na hivyo majirani zake ndio waliomuokoa mkewe……
Hata hivyo baadhi ya majirani walioongea na mwandishi wamedai kuwa wawili hao ( Upunguvuku na mama Maua) ni wapenzi wa siku nyingi na wamekuwa wakionekana mara kadhaa wakienda kunywa pombe za kienyeji…..
“Huyu Upunguvuku ni fundi Mwashi, tunamfahamu vizuri kuwa ni hawara wa mama Maua, mara kadhaa huwa tunawaona wakinywa pombe za kienyeji pamoja, sema tu leo wamefumwa wakijivinjari ndo mwanamke anamsingizia eti kambaka,” alisema shuhuda mmoja.
Juhudi za kumpata Kingwendu kuongelea mkasa huo hazikuzaaa matunda kutokana na simu yake kutopatikana kila akipigiwa
Maoni
Chapisha Maoni