RAY: Nimerudi sasa Kazini
0
MUONGOZAJI na mwigizaji mahiri katika tasnia ya filamu Swahilifilamu Vincent Kigosi ‘Ray’ amesema kuwa hajatoweka katika tasnia ya filamu bali alikuwa akijipange kwa ajili ya kuangalia soko la kimataifa kwani soko la ndani tayari wamelishika.
Ray anasema kuwa wapenzi wa kazi zake wajiandae kupokea kazi mpya ambazo zipo tayari zinakuja huku akiwa ameendelea na mpango wake wa kuendelea kuibua vipaji vipya ambavyo vitakuwa nyota baada ya kazi hizo kutoka.
“Samahani sana wadau wangu, naombeni sana mnisamehe kwa kupotea kwa kipindi kirefu, na yote haya yanatokana na majukumu ya kufanya kazi kimataifa zaidi, soko la ndani tumefanikiwa, nisingependa kuja kwenu na mikono mitupu, hivyo mtarajia kazi zenye ubora”anasema Ray
Maoni
Chapisha Maoni