NANDO amkera LULu ile mbaya; tazama picha hapo chini
MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibuka na kufunguka kuwa amekerwa na kitendo cha mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa (BBA) 2013, Amir Khan Nando kujinadi kuwa aliwahi kuwa ‘mtu’ wake kitu ambacho si cha kweli.
Akizungumza na Ijumaa kwa juzikati, Lulu alikiri kuwa Nando aliwahi kumtokea na alimkubalia awe ‘my baby’ wake lakini baada ya kumshtukia kuwa hana nia nzuri, alimpotezea kabla hawajazama kwenye dimbwi la mahaba.
Juzikati, Nando alifanya mahojiano na Global TV Online ambapo awali alidai ‘kutembea’ na Lulu lakini alipobanwa zaidi aliumauma maneno na kudai anampenda na yuko tayari kumuoa kwa sababu ana sifa za kuwa mke (wife material).
Ili kuyapata mahojiano kamili ya Nando, tembelea tovuti ya utaona bango la Global TV, bofya hapo na utapata majibu mengi ambayo staa huyo wa BBA alifunguka pamoja na vipindi vingine vya kusisimua.
Maoni
Chapisha Maoni