Matatani kwa kuwinda katika shamba la Mugabe


Rais Robert Mugabe
Jirani yake Rais wa Zimbabwe Robert, ametozwa faini kwa kuwinda katika shamba la ras huyo.
Mahakama ilimuauru Michael Pazarangu, ambaye aliwapeleka Mbwa wake kuwinda mnyama anayejulikana kama Mbawala au 'Deer' katika shamba la Mugabe, kulipa faini ya dola 50 au afungwe jela kwa siku thelathini.
Kwa mujibu wa gazeti la serikali la Herald, Bwana Pazarangu alituhumiwa kwa kuwaruhusu Mbwa wakali kuingia katika shamba binafsi la Rais Mubage, mjini Harare.
Mubage ambaye ana umri wa miaka 90, amekuwa mamlakani tangu Zimbabwe kujitawala 1980.
Alichaguliwa tena mwaka jana na kumshinda hasimu wake wa jadi Morgan Tsvangirai.
Mtuhumiwa Pazarangu, alikiri kosa lake kinyume na alivyokuwa amesema hapo awali ambapo alikanusha madai hayo.
"kesi hii imewagusa watu wengi na imeniathiri sana,'' alinukuliwa akisema Bwana Pazarangu
Mahakama iliambiwa kuwa Mbwa wa mtuhumiwa walimuua Mbawala katika shamba la Mugabe mwezi Mei mwaka 2013 katika eneo la Borrowdale .
Mbwa hao walisemekana kuingia katika shamba la Mugabe kupitia ukuta unaogawanya nyumba za wawili hao.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SASA HII NI NGONO BONGO MUVI.... Video ya Irine Uwoya na Rich wakifanya YAO..LIVE

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

BEIJING DAXING: UWANJA MKUBWA WA KIMATAIFA WA NDEGE CHINA WAFUNGULIWA, HATARIIII!