BRAZIL NAYO ETI YATINGA NUSU FAINALI KWA MBINDE KUCHUANA NA UJERUMANI NUSU FAINALI JULY 08, 2014
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Brazil imejikatia tikiti ya nusu fainali ya kombe la dunia baada ya kuilaza Colombia mabao 2-1 katika mechi ngumu ya robo fainali.
Kufuatia ushindi huo Brazil sasa watachuana na Ujerumani katika nusu fainali iliyoratibiwa kuchezwa Jumanne ijayo Julai tarehe 8.
Taarifa zinazohusiana
Kama ilivyo tarajiwa vijana wa Luiz Felipe Scolari ambao ''wana mkono mmoja kwenye kombe la dunia kulingana na kocha huyo'' walitangulia kuweka niya yao wazi kunako dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza Thiago Silva alipofunga kwa kichwa mkwaju ambao ulimwacha kipa machachari David Ospina asijue la kufanya .
Baada ya kipindi cha pili kwanza ,Colombia walikuwa mbioni wakitafuta bao la kusawazisha dhidi ya wapinzani wao waliofurahia umati wa nyumbani ,Ghafla bin vuu Brazil wakaongeza bao la pili kupitia kwa mkwaju wa Freekick wa David Luiz kunako dakika ya 69 ya kipindi hicho cha pili .
Kuanzia hapo Brazil ilianza kulinda ngome yake dhidi ya wimbi baada ya wimbi ya mashambulizi kutoka kwa Colombia.
Bao la kufutia machozi la Colombia lilipachikwa kimiani kupitia mkwaju wa penalti kipa wa Brazil Julio Cesar alipomwangusha James Rodriguez katika eneo la lango.
Rodriguez aliutia kimiani na kusajili bao lake la sita.
Mshambulizi huyo wa Colombia ndiye anayeongoza katika ufungaji mabao huko Brazil.
Awali Thiago Silva alioneshwa kadi ya njano na hivyo hataweza kushiriki mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani siku ya jumanne .
Taharuki ilitanda uwanjani na kwa ukumbwa Brazil nzima baada ya nyota wao Neymar kuondolewa kwa haraka uwanjani na kukimbizwa hospitalini baada ya kujeruhi uti wa mgongo na Juan Camilo Zuniga.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni