Obama: Kombora ndilo liliangusha ndege ya Malaysia huko Ukraine
Rais Barack Obama wa Obama anasema ushahidi unaonesha kuwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia iliyoanguka mashariki mwa Ukraine ilitunguliwa kwa kutumia kombora lililofyetuliwa kutoka nchi kavu kuelekea angani kutoka eneo linalodhibitiwa na waungaji mkono wa Russia wanaotaka kujitenga.
Akizungumza White House Ijumaa, Rais Barack Obama aleleza vifo vya watu 298 waliokuwemo ndani ya ndege kua ni ‘jambo la kuchukiza lisiloweza kuelezeka’. Alieleza raia mmoja wa Marekani miongoni mwa waliokufa, kufuatana na habari walizopokea hadi wakati huo.
Kiongozi wa Marekani alisema " hayo ni maafa ya kimataifa, pale ndege ya nchi ya Asia kuharibiwa juu ya anga ya Ulaya ikiwa na raia wa mataifa mbali mbali. Kwa hivyo ni lazima kufanyike uchunguzi wa kuaminika wa kimataifa."
Rais Obama, aliongezea kusma kuwa ili kufanikisha uchunguzi, Russia, kundi la waasi wanaotaka kujitenga pamoja na Ukraine lazima wasitishe mapigano mara moja. "Huu ni wakati wa kudumisha tena amani na usalama Ukraine."
Ndege ya Shirika la Malaysia MH17 ilikuwa njiani kutoka Amsterdam kuelekea Kuala Lumpa wakati shambulizi la anga lilipotokea.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Lakutana
Akizungumza kwnye kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa, Ijumaa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power alisema chombo cha kufyetua kombora huwenda kilikuwa katika "eneo linaloshikiliwa na waasi mashariki ya Ukraine."
Akieleza kwamba haimkiniki waasi wanauwezo wa kutumia chombo hicho bila ya msaada kutoka mtu mwenye kufahamu vyema namna ya kufyetua makombora hayo.
Wakati huo huo balozi wa Ukraine katika Umoja wa Mataifa, Yuriy Sergeyev alisema Ukraine itawasilsha ushahidi kwa baraza hilo unaoonesha jeshi la Russia lilihusika katika ajali hiyo.
Serikali ya Ukraine awali iliwashutumu waungaji mkono wa Russia wanaotaka kujitenga kwa kutengua ndege huku waasi wakilaumu majeshi ya serikali. Russia inakanusha kuhusika kaika tkio hilo.
Abiria wengi waliokuwa kwenye ndege hiyo ya aina ya Boeing 777 walikuwa wa-Holanzi na wengi walikuwa wanasayansi wanaoelekea kwenye mkutano wa kimataifa wa ukimwi nchini Australia.
Bwana Obama alisema Ijumaa kuwa Marekani iko tayari kutoa msaada wa aina yeyote ikibidi. Alisema wafanyakazi wa FBI na NTSA tayari wapo njiani kuelekea katika eneo la ajali ambako kuna mabaki ya ndege hiyo na miili ya abiria ambao haijaondolewa bado.
Maoni
Chapisha Maoni