Tanzania: Frederick Sumaye kugombea urais 2015
Nchini Tanzania, siku chache baada ya mwanasiasa kijana na naibu waziri January Makamba kutangaza nia ya kugombea urais mwaka 2015, sasa waziri mkuu wa zamani Frederick Sumaye amejitokeza akisema atagombea wadhifa huo.
Zaidi kuhusu tangazo hilo la Sumaye na kile kinachoonekana kuwa ni kuanza kinyang'anyiro katika chama tawala nchini Tanzania CCM, anaripoti mwandishi wetu Guiji la habari. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Maoni
Chapisha Maoni