Uchawi wa Ajabu: Picha za Ndege aliyekuwa Anapaa na kugeuka kuwa Mwanamke


Mapema wiki hii katika kijiji cha Oshindi nchini Nigeria wananchi walishuhudia sinema ya  bure  ambapo kamera zao zilikuwa macho yao na simu zao pale ndege aliyekuwa anapaa angani ghafla alianguka chini baada ya kudandia nyaya za umeme na kugeuka mwanamke.
 
Kitendo hicho kiliwaacha wananchi vinywa wazi wasijue la kufanya huku wakibaki kupiga picha kwa  kutumia simu zao za mikononi.
 
Mwanamke huyo alionekana kuchubuka na kuwa na vidonda katika mwili wake hali iliyo kuwa inahuzunisha huku akiwa haongei (bubu) .
 
Wananchi hao walimuuliza maswali  mengi wakitaka kujua imekuaje hadi akageuka binadamu wakati yeye alikuwa ndege anapaa juu.
 
Mama huyo aliwajibu kuwa alikuwa anaenda kumtazama binti yake aliyekuwa amejifungua muda mchache.
 
Habari zinasema kuwa mwanamke huyo alikuwa mchawi na binti yake alikuwa anafanya sala wakati yule mama alikuwa anapaa.
MCHAWI
 
Inaelezwa kuwa wakati sala inaendelea ndipo mwanamama  huyo aliyekuwa  amejibadilisha  na  kuwa  ndege akageuka binadamu.
 
Taarifa  zinaarifu  kuwa binti yake alikuwa kila akijifungua,  mtoto anafariki papo hapo.
 
 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.