JACQUELINE WOLPER AFYATA MKIA...AMWANGUKIA YULE PEDESHEE WA KIKONGO!

Staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe. Kikizungumza na Risasi Mchanganyiko, chanzo makini kilidai kwamba baada ya gazeti ndugu na hili kuripoti habari ya Wolper kumchana Mkongo huyo huku akidai hana hadhi ya kuwa naye, wiki iliyopita alionekana kwenye Hoteli ya Double Treeiliyopo Masaki jijini Dar ambako ndipo alipofikia mwanaume huyo. Kiliendelea kueleza kwamba mwanadada huyo alifika hotelini hapo kwa ajili ya kumuomba msamaha Mkongo na alikuwa akifanya jitihada kubwa ili asamehewe kwa kumtumia mwanamuziki wa FM Academia, raia wa Kongo, Patcho Mwamba amuombee msamaha.
BAADA ya hivi karibuni kumchana laivu Mkurugenzi wa Mwami Foundation, raia wa Kongo, Mwami Rajabu, staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kumwangukia jamaa huyo na kumuomba msamaha. 


“Nimemuona Wolper akiwa na huyo Mkongo kwenye hoteli hiyo aliyofikia ambapo kilichompeleka ni kuomba msamaha kutokana na maneno aliyozungumza kwenye gazeti,” kilisema chanzo hicho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.