Mtandao mpya wa kijamii 'Ello', mpinzani mkuu wa Facebook, Jiunge hapa

Wakati dunia ukiuchukua mtandao wa Facebook kama mtandao wa kijamii wenye watu wengi na uliosambaa zaidi duniani, mtandao huo umepata mpinzani mkubwa ambaye anachukuliwa na wengi kama mbadala wake, ‘Ello’.
Mtandao wa Ello uliotengenezwa na Paul Budnitz umetimiza wiki nane tu tangu uanze kutumika na maelfu ya watu wameendelea kujiunga ndani ya muda mfupi.

Baadhi ya watumiaji wa mtandao huo wameukosoa mtandao wa Facebook kuwa sio mtandao bora wa kijamii na kwamba umejikita zaidi katika kufanya biashara kupitia matangazo tofauti na ilivyo kwa ‘Ello’ ambao haulipishi kiasi chochote cha fedha kwa matangazo.
Mwanzilishi wa Ello amekaririwa akisema kuwa anaona Facebook kama mtandao uliojikita zaidi kwenye kufanya matangazo badala ya kuwa mtandao wa kijamii.
Mtandao huo umebatizwa jina la ‘Anti-Facebook’.
“Kila kitu kiko kwenye mpangilio mzuri wa mfuatano. Watu wataona kile tu wanachotaka kuona.” Amesema muanzishi wa Ello, Budnitz.

Mwanzilishi wa Ello, Paul Budnitz
Je ni kweli Ello itaifunika Facebook? Bofya hapa kujiunga
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.