Cloud Afunguka Baada Ya Tuhuma za Kumfanyia Fitina Frank Mwikongi Deal La Uingereza.


Cloud
Msanii mkongwe wa filamu Tanzania Issa Musa ‘Cloud’ amekana tuhuma zinazosambazwa mtandaoni kuwa alimfitini muigizaji mwenzake, Mohammed Mwikongi ‘Frank’ ili kumzuia asisafiri kuelekea Uingereza miezi michache iliyopo.

“Mimi sikumfitini Frank, yule mtu alinifuata mwenyewe kwa makubaliano ya mdomo kuwa nikacheze filamu, sikuwa peke yangu, tuliongozana na kina Monalisa na Riyama, tatizo ni la huyo aliyenipeleka kule, nilifanya mambo kwa mazoea na ndiyo sababu anaamua kusambaza uongo dhidi yangu,” alisema Cloud  wakati akizungumza na Globalpublishers
Cloud aliwasihi wasanii wenzake nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wahakikishe wanaingia mikataba ya maandishi ili wawe na ushahidi wakati waliokubaliana nao kazi wanapoleta ujanjaujanja kama ilivyomtokea yeye katika safari hiyo ya Uingereza ambayo sasa inamletea uadui na Frank.

                                                         Frank

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.