BREAKING NEWS! WABUNGE KUMI NA SABA (17) WAACHIA NGAZI:

Wakati Mh. Rais Kikwete, leo tarehe tisa Julai anategemewa kulivunja rasmi Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa rasmi zinasema kuwa wabunge kumi na saba wameachia rasmi nafasi zao na hawata gombea tena nafasi ya Ubunge katika Mabunge yajayo.

Kati ya hao, kumi na sita ni kutoka chama tawala yaani CCM na mmoja ni kutoka chama rasmi cha upinzani Bungeni yaani CHADEMA. aidha wabunge wawili wa CHADEMA wametangaza kujitoa uanachama wa CHADEMA mara baada ya Bunge hilo kuvunjwa.

Waliotangaza kutogombea tena nafasi ya Ubunge katika Bunge la Muungano, kutoka CCM ni hawa wafuatao;-
1. Michael Lekule (Longido),
2.Mohamed Dewji (Singida Mjini),
3.Deogratius Ntukamazina (Ngara),
4. Mohamed Misanga (Singida Magharibi),
5.Maria Hewa (Viti maalumu),
6. Mizengo Pinda (Mlele),
7.Edward Lowassa (Monduli),
8. Bernard Membe (Mtama),
9. Samweli Sita (Urambo),
10. Anna Makinda (Njombe Kusini),
11. Mark Mwandosya (Rungwe Magharibi),
12. Balozi Seif Idd ( Kitope),
13. John Nchimbi (Songea Mjini),
14. Eustace Katagira (Kyerwa),
15. John Chiligati (Manyoni Mashariki),
16. Hezekiah Chibulunje ( Chilonwa).
Sababu kubwa waliyo toa waheshimiwa hawa ni kwamba wametumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 15 hadi 20, hivyo wameona ni wakati muafaka kwa fikra na sura nyingine kuingia Bungeni.

kwa upande wa cha CHADEMA, aliyetangaza kutogombea ni Mh. Philemoni Ndesamburo, aidha wabunge wawili wa CHADEMA wametangaza kujitoa CHADEMA mara Rais atakapo vunja Bunge leo;- Hao si wengine bali Mh. Said Amour Arf (Mpanda Kati) na John Magele Shibuda (Maswa).

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.