BREAKING NEWS!! BERNARD MEMBE AJIUZULU SIASA NCHINI TANZANIA, NI BAADA YA KUONDOLEWA KUGOMBEA URAISI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, amesema hatogombea wadhifa wowote kwenye uchaguzi mkuu ujao nchini humo na kwamba anapanga kujishughulisha na masuala yake ya kibinafsi.
Membe ambaye alikuwa akitafuta tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania urais mwezi Oktoba lakini akashindwa kufikia lengo hilo, amesema kuwa, hatotafuta nafasi ya ubunge katika jimbo lake la Mtama.
Hata hivyo amesema ataendelea kukiunga mkono chama chake cha CCM na atampigia debe mgombea urais aliyeteuliwa na chama hicho, Bw. John Magufuli.
Awali kulikuwa na tetesi kwamba Membe angegombea ubunge baada ya kukosa nafasi ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM.
Huku hayo yakijiri, chama tawala nchini Tanzania kinaendelea kupata pigo baada ya baadhi ya wabunge wake kutangaza kuwa hawatogombea tena nafasi zao kupitia chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao. 
Mbunge wa Kahama, James Lembeli ni mwanachama wa CCM wa hivi karibuni kutangaza kuwa hatatetea kiti chake kupitia chama hicho kwenye uchaguzi wa Oktoba mwaka huu. 
Tayari madiwani 20 wa CCM katika jimbo la Monduli wametangaza kuhamia Chadema na kumtaka mbunge wao, Edward Lowassa kufuata mkondo huo.
CHANZO: TEHRAN KISWAHILI

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.