Muda Sahihi Wa Kufanya Mapenzi Ni Upi?
Somo hili linaweza kukushangaza msomaji wangu, kutokana na ukweli kwamba ufanyaji mapenzi, hauwezi kuupangia muda, lakini katika hali ya kawaida ipo tofauti kubwa ya kufanya mapenzi, mchana, usiku, alfajiri na nyakati za joto na kelele nyingi za wapita njia. Utofauti huu ndiyo unaweza kutofautisha hali ya kufurahia tendo kati ya mtu na mtu. Hakuna ubishi kwamba watu wanaofanya mapenzi nyakati za joto, hupoteza msisimko wa tendo si tu kwa sababu ya kuchoka haraka bali hata kwa kukinai harufu ya jasho liwatokalo mwilini. Sababu hiyo na nyingine nyingi, zitokanazo na kutojua muda sahihi wa kufanya tendo la ndoa, zimewafanya wapenzi wengi kushindwa kuridhika au kupata raha stahili wakati wa kujamiiana na wapenzi wao, jambo ambalo linanipa sababu ya kufundisha muda sahihi wa kufanya mapenzi ni upi? Kwa mujibu wa uchunguzi wa wataalamu wetu, ambao pia ulitiwa nguvu na machapisho mbalimbali yaliyotolewa kwenye magazeti ulibainika kuwa muda muafaka wa wapenzi kufanya tendo l...