Rais John Pombe Magufuli Amtumbua Jipu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji TIC


Aliyekuwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bi. Juliet Kairuki kuanzia tarehe 24 Aprili mwaka huu.


Taarifa iliyotolewa na kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, imesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya rais Dkt. Magufuli kupata taarifa kuwa Mkurugenzi huyo alikua hachukui mshahara wa serikali tangu alipoajiriwa mwaka 2013 jambo ambalo linazua maswali mengi.


Aidha, taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu huyo imeongeza kuwa endapo Bi. Kairuki atakuwa tayari kuendelea kufanyakazi na Serikali ya Awamu ya Tano atapangiwa kazi nyingine. Mchakato wa kumpata Mkuregenzi mpya umeanza mara moja.


Kwa mujibu wa Prof. Mkenda kwenye taarifa yake hiyo amesema Bw. Clifford Katondo Tandali, atakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho cha Uwekezaji

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA