AFISA TARAFA WA KIBITI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA



pol
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Boniventura Mushongi akizungumza na waandishi wa habari kuhusina na tukio la kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Afisa Tarafa wa Kibiti kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa  la sita katika shule ya Kitunda.(Picha na Victor Masangu)
NA VICTOR MASANGU,  PWANI
JESHI la  polisi Mkoa wa Pwani limemkamata na kumfikisha mahakamani  Afisa Tarafa wa Kibiti Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani Selemani  Mpangile almaarufu babu konyeza kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita 
katika shule ya msingi kitunda.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi  ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Boniventura Mushogi amesema kwamba tukio hili limetokea juzi majira ya saa 10 jioni ambapo mtuhumiwa aliamua kutenda kosa hilo kinyume na sheria na  taratibu za nchi.
Mushongi alisema kwamba jeshi la polisi  litaendelea kuvalia njuga vitendo vya ubakaji kwa watoto wadogo kwani kunaweza kuwasababishia madhara makubwa watoto hao kutokana na kufanyiwa vitendo kama hivyo wakiwa na umri mdogo.
Kamanda Mushongi amefafanua kuwa tukio hilo la ubakaji mtuhumiwa alilifanya katika ofisi yake wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akipita nje ya jengo hilo na ndipo alipomwita na kuingia ndani ambapo alimziba mdomo wake kwa koti  leke ili asipige kelele kasha kutekeleza azma yake ya kumbaka .
Katika hatua nyingene Kamanda ametoa onyo kwa wanafunzi kuachana  na tabaia ya kuwa na tamaa ya kupenda vitu vya bure, na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawatunza na kuwalea watoto wao katika misingi mizuri ya kimaadili na sio kuwa na fikra potofu.
“mimi napenda kutoa onyo kwa wanafunzi na watoto waache kabisa tabia ya kuwa na tama, kwani wakifanya hivyo matokeo yake ndio hayo kwani wakati mwingine wanapenda vitu vya bura kama pipi, soda kwa hivyo hii ni hatari sana, pia na wazazi wahakikishe wanawalinda watoto wao,” alisema Mushongi.
MATUKIO ya vitendo vya ubakaji kwa watoto wadogo katika Mkoa wa Pwani bado yanaonekana  kuwa ni tatizo kubwa hivyo kunahitajika juhudi za makusudi zifanyike na serikali katika kuwachukulia hatua kali za kisheria na kutoa adhabu kali  kwa wale wote watanaobainika kuhusika  katika matukio kama hayo.(P.T)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.