Mwanri Aagiza Wahusika Watumishi Hewa Kukamatwa


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri, ametoa siku saba kwa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na wakuu wa wilaya kuorodhesha idadi ya wafanyakazi waliopo katika maeneo yao na kuwakamata wale wote wanaotuhumiwa kuisabishia serikali hasara.

Bw. Mwanri amesema pamoja na kurejeshwa kiasi cha shilingi milioni 54 kati ya shilingi milioni 118, walizolipa mishahara hewa wafanyakazi 48 waliobainika hapo awali lakini mkakati madhubuti unahitajika wa kurejesha zaidi ya shilingi milioni 63 zilizobakia ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.

Mwanri ametoa maagizo hayo wakati wa kikao kati yake, na Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za wilaya, Maafisa Utumishi, Tawala na Elimu, ngazi za wilaya na mkoa kutoa wilaya zote za mkoa wa Tabora.

Katika hatua nyingine katika kikao hicho Mkuu huyo wa mkoa wameitaka kila halmshauri kukamilisha utengenezaji wa madawati kwa kila shule na kusema hadi Mei 30 zoezi hilo liwe limekamilika.

Kwa upande wao baadhi ya Wakurugenzi na Watendaji wa Halmashauri za wilaya wameahidi kutekelza agizo hilo na kusema kuwa tayari wameshaanza kufikia hatua kubwa katika kutatua tatizo hilo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.