Edward LOWASSA Ajitokeza na Kumkosoa Rais Dr John MAGUFULI, Amuhoji Maswali Matatu Mazito!


Aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, amehoji maswali matatu kwa Rais Dk. John Magufuli.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Lowassa amemtaka Rais Magufuli baada ya kusema hakuna mtoto atakayelipa ada kuanzia Januari, mwakani, atamke mustakabali wa wanafunzi walioko shuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.

Lowassa amesema kwa upande wake ahadi ya elimu bure aliyokuwa akiinadi wakati wa kampeni, ilikuwa ni kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu na kwamba hata wale walioko mashuleni, wangeguswa na hatua hiyo.

“Niliahidi watoto wote walioko na watakaoanza shule kuanzia kindergarten (shule ya awali) hadi chuo kikuu, serikali yetu ingegharimia. Na nilitangaza kufuta michango yote shuleni ili kumpunguzia mzigo mwananchi,” alisisitiza Lowassa ambaye amekataa kuyatambua matokeo ya ushindi wa Dk. Magufuli akidai kuwa yeye ndiye aliyeshinda kwa asilimia 62 ya kura zote zilizopigwa.
Kuhusu suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, Lowassa amesema yeye alishaweka wazi kuwa elimu ingekuwa bure hadi chuo kikuu.
“Vijana hawa wanahangaika na mikopo na nasikia ni asilimia 17 tu kati ya wanafunzi 70,000 ndiyo waliopata mikopo. Sera ya Chadema na Ukawa kwa ujumla, ni kufuta kabisa shida hizi kwa serikali kufadhili elimu yao,” alifafanua Lowassa katika taarifa yake hiyo.

Kwa msingi huo, Ukawa kupitia kwa aliyekuwa mgombea wao wa urais, Lowassa, umewataka wananchi kutofautisha ahadi ya elimu bure iliyotolewa na Rais Magufuli na ile iliyotolewa na Ukawa.

Lowassa alisema Magufuli ametoa maelekezo kwa watendaji wa serikali kuweka mikakati ya kutekeleza ahadi yake kuanzia Januari, mwakani kwamba hakuna mtoto atakayelipa ada.
Hata hivyo, amesema hajaeleza waziwazi hatma ya wanafunzi walioko mashuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.