FRANK AMLALAMIKIA RIYAMA KUMZIBIA RIZIKI


Nyota wa filamu za Kibongo, Mohammed Mwikongi maarufu kama Frank.
NYOTA wa filamu za Kibongo, Mohammed Mwikongi maarufu kama Frank, amedai kuwa msanii mwenzie Riyama Ally anamzibia riziki kiasi kwamba sasa anamsaka ili amweleze kitu gani aliwahi kumkosea.
Akizungumza jijini hivi karibuni, Frank alisema anamtafuta Riyama ili aweze kumwambia ni kwa nini inakuwa hivyo kwa sababu katika filamu zote ambazo yeye anatakiwa kucheza, mwenzake huyo huwepo na ndiye anayependekeza watu watakaohusika na filamu hiyo.
“Tukiacha ile filamu iliyofanyika nchini Uingereza ambayo iliandaliwa na Dida Entertainment, kuna filamu nyingine iliandaliwa na Mbunge Shamsa Mwangunga ambaye alinipigia simu na kuniomba nicheze nafasi aliyoipendekeza lakini baada ya siku, nafasi yangu ikachukuliwa na Slim.
Msanii wa filamu Bongo, Riyama Ally.
“Pia kuna nyingine ambayo iliandaliwa na mtu wa mtaani kwetu ambaye ni mfuatiliaji mzuri wa kazi zetu, nafasi yangu ikachukuliwa tena na Msungu, sasa mimi namtafuta Riyama aniambie ni kwa nini huwa ananizibia riziki yangu wakati imeshapangwa,” alisema.
Riyama hakuweza kupatikana kupitia simu yake ya mkononi kwani mara zote iliita bila kupokelewa. Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno haukujibiwa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.