LATIN AMERIKA YATEKA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Beki wa Honduras, Maynor Figueroa (kushoto) akimtazama beki wa Ecuador, Jorge Guagua (katikati) akipiga kichwa wakati wa mchezo wa Kundi E uliozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Baixada, Curitiba jana. Ecuador ilishinda 2-1. Picha na AFP 

KWA UFUPI
Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini timu sita za Amerika Kusini zilifuzu kwa hatua ya mtoano

Sao Paulo, Brazil. Hadi sasa Kombe la Dunia 2014 ni moja ya fainali zenye mambo mengi ya kukumbukwa. Kumeshuhudiwa mabao mengi, matokeo mengi ya kushangaza na miamba miwili yaa Ulaya, Hispania na England tayari wameaga mashindano hayo.
 Kwa upande wa pili, ukiondoa Honduras, timu za mataifa ya Latin Amerika zimeng’ara katika fainali hizi.
Colombia na Chile tayari zimefuzu kwa hatua ya mtoano kwa kuonyesha kiwango cha juu na kushinda mechi zao mbili.
Nayo Costa Rica imefuzu kwa hatua ya 16 baada ya kuwaduwaza mabingwa mara nne Italia kwa ushindi wa bao 1-0.
Ushindi wa Costa Rica si tu ni wa kihistoria kwa nchi hayo ya CONCACAF bali ni ishara njema katika historia ya nchi za Latin Amerika.
 Kombe la Dunia hili linaweza kuwa la kwanza kwa nchi za Amerika Kusini kuingiza timu saba katika hatua ya mtoano.
Mara ya mwisho nchi nyingi za Latin Amerika kufuzu kwa hatua ya 16 ya Kombe la Dunia zilikuwa nchi sita katika fainali za Afrika Kusini 2010 (Brazil, Chile, Argentina, Mexico, Uruguay, na Paraguay). Sasa, Brazil kunaweza kuwa na timu saba za Latin Amerika katika hatua hiyo ya mtoano.
Jinsi Latin Amerika walivyoteka Kombe la Dunia:
Brazil ina uhakika wa kufuzu kwa hatua ya 16, wakati watakapocheza mechi ya mwisho na timu dhaifu ya Cameroon. Argentina inaonekana ni bora zaidi katika Kundi F. Tayari , Chile, Costa Rica na Colombia zimefuzu. Kama Uruguay itaifunga Italia, na Mexico wakifanikiwa kushinda au kupata sare dhidi ya Croatia hiyo itamaanisha timu saba za Latin Amerika zitakuwa zimefuzu kwa mtoano.
Pia, Marekani inaweza kuongeza idadi hiyo ya timu kama itafuzu, pamoja na Ecuador kama itashinda dhidi ya Ufaransa zote zitafuzu kwa mtoano.
 Kwa mazingira hayo sasa Latin Amerika inapewa nafasi kubwa ya kulibakiza taji hilo kama walivyofanya wakati fainali hizo zilipofanyika barani humo miaka ya 1930, 1955, 1962, 1970, 1978 na 1986.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.