Video ya NdiNdiNdi Imemrudisha Mwanamuziki Jide kwa Director Campos wa South Africa

Baada ya miaka 10 ya kufanyakazi na muongozaji wa video Justin Campos, Komando Jide au Lady Jaydee amerudi tena kwake kufanyanaye kazi, kutengeneza video ya wimbo wake wa #NdiNdiNdi

Taarifa hiyo ya kufanyakazi na Justin Campos ameitoa Lady Jaydee mwenyewe kwenye ukurasa wake wa Instagram, baada ya kupost video ikimuonyesha Justin Campos akisema ni heshima kwake kufanyakazi na Jaydee ingawa si mara ya kwanza.

“Nilikutana na Justin Campos kwa mara ya kwanza 2006 wakati tunafanya video ya 'Njalo' nilioshirikiana na kundi la Afrika Kusini linalojulikana kama 'Mina Nawe', Justin ndio alikuwa Director wa video hiyo baada ya miaka 10 tumefanyanae kazi tena 2016,” aliandika Jaydee.

Pia Lady Jaydee ameanza kupost picha za video hiyo huku akiandika “#NdiNdiNdi loading Kikomandooooooo #NguvuYaUmma #WananchiWameipokea #NdiNdiNdiMusicVideo”

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA