HUU NDO MSHAHARA ANAOLIPWA MBWANA SAMATTA NCHINI UBELIGIJI
Najua unatamani kujua maisha ya wanasoka wa Ubelgiji hususani katika kipindi hiki anachocheza soka mtanzania Mbwana Samatta nchini humo, kiukweli mshahara wa Samatta haupo wazi katika vyombo vya habari, ila Ligi ya Ubelgiji wachezaji wanalipwa kwa mwezi.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.xpats.com hadi kufikia April 10 2015 mishahara ya wachezaji wengi wa Ligi Kuu Ubelgiji
ilikuwa inatajwa kuwa ya wastani wa euro 253,586 kwa mwaka ambazo ni
zaidi ya milioni 600 za kitanzania kabla ya kukatwa kodi pamoja na bima.
Kwa mwezi huwa inatajwa kufikia wastani wa euro 20000 ambazo ni zaidi ya milioni 45 za kitanzania. Klabu ya Anderlecht iliyopo nafasi ya tatu katika Ligi, ndio inatajwa kuwa klabu inayolipa mishahara mikubwa zaidi, kwa mwaka Anderlecht inalipa hadi euro 600000 ambazo ni zaidi ya bilioni 1.4 za kitanzania kwa mchezaji mmoja.
Klabu ya KRC Genk anayocheza nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta inatajwa kuwa miongoni mwa vilabu tajiri ndani ya Ligi Kuu Ubelgiji, ila kwa mujibu wa www.xpats.com, wachezaji wengi wao Ubelgiji hulipwa
kati ya euro 25000 hadi 50000 kwa mwezi.Kwa hiyo samatta mshahara kwa
pesa ya kitanzania utakuwa kati ya milioni 50 hadi milioni 70 kwa mwezi
Maoni
Chapisha Maoni