Ukweli wa kaka’ke Diamond kubaka Sweden

 Mwisho wa utata? Hatimaye ukweli juu ya sakata la kaka wa staa wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Rommy Jones umeanikwa ndani ya Ijumaa Wikienda ambalo ni namba moja kwa habari za mastaa ndani na nje ya Bongo.
Kabla ya gazeti hili kuchimba undani wa msala huo, kulienea tetesi mbalimbali kuwa Rommy ambaye ni DJ rasmi wa Diamond na mmoja wa wafanyakazi wa Wasafi Classic Baby (WCB) kuwa amebaka kisha kukimbia nchini humo bila kuelezwa undani wa tukio hilo.
WIKIENDA MZIGONI
Katika kusaka undani wa sakata hilo, wikiendi iliyopita Ijumaa Wikienda lililazimika kuzungumza kwa nusu saa na Meneja Matukio ya Kimataifa wa Diamond, Sallam Sharaff.
Akisimulia kilichotokea, Sallam alisema kuwa maneno yaliyozagaa mtaani na kwenye mitandao ya kijamii yalielemea kwenye ushabiki na hata yanavyoelezewa hakuna anayetambua undani wa tukio hilo lilivyojiri.
Sallam alisema, ukweli wa kila jambo wanafahamu zaidi familia ya Wasafi, hasa wote waliokuwepo kwenye Ziara ya Ulaya.
BOFYA HAPA KUMSIKIA SALLAM
“Mara kadhaa nimekuwa mzito sana kuongelea suala la Rommy Jones kufuatia baadhi ya watu kulichukulia tofauti kabisa na ilivyotokea.
“Ishu hiyo ni kweli ilitokea lakini ninachoweza kusema ni kwamba ulikuwa ni mchezo mchafu ambao ulilenga kuichafulia jina WCB.
“Madai ya Rommy Jones kubaka siyo ya kweli kwa sababu mimi ninachokijua ni kwamba, huyo mrembo aitwaye Debora alikuwa akiwasiliana na Rommy Jones siku kibao yaani ni zaidi ya miaka miwili huko nyuma.
diamond33Rommy akiwa na Diamond.
WATUA SWEDEN, DEBORA AJUA
“Siku tulipofika Sweden tu, Debora alijua kuwa Rommy Jones yupo ‘so’ alimnunulia zawadi ya simu na kumletea kwenye apartments (nyumba za kuishi) tulizokuwa tumefikia na jioni yake akamtumia gari, likaja kumchukua na kumpeleka kwake.
“Kusema kweli sisi huko nyumbani kwa Debora hatukupafahamu ila siku hiyo alimrejesha mapema, tena wakiwa na furaha ya hali ya juu.
“Sisi wote tukaanza kumtambua kama shemeji yetu hivyo jambo la kubakwa hapo sijui linatokea wapi…
“Ukiachilia mbali hiyo, siku iliyofuata mimi nilikuwa nimetoka, baada ya kurudi muda wa jioni sikumkuta Rommy Jones, nilipoulizia nikaambia Debora amemchukua na kuondoka naye.
“Alilala huko na kurudi asubuhi yake maana tulikuwa tunaenda kufanya shoo kwenye mji mwingine.
MCHEZO MCHAFU?
“Ujue ishu hii mimi baadaye nilikuja kugundua kwamba kuna namna ambayo Debora alikuwa akitengeneza mazingira ya kutafuta pesa kwani sheria ya Sweden siku zote ukilala na mwanamke bila ridhaa yake akishitaki unatuhumiwa kuwa umebaka na yeye analipwa kama dola elfu kumi na mbili (zaidi ya Sh. milioni 24 za Kitanzania).
HATA MKEO?
“Hata kama ni mkeo, ukifanya naye tendo la ndoa bila yeye kuridhia na akashitaki, basi wewe utakuwa umebaka na sheria inakufunga huku yeye akilipwa kiasi hicho cha fedha.
salam menejaMeneja wa Diamond, Sallam Sharaff.
KILICHOTOKEA SASA
“Kilichotokea kwa Rommy Jones ni dhahiri kabisa kuwa Debora alitaka kujipatia pesa kwa njia hiyo kwani baada ya kuanza kung’aka kuwa amebakwa, mimi nilimtafuta na kumuomba msamaha maana Rommy Jones hakujua kama sheria ya huko iko hivyo na isitoshe wote walikuwa wamelewa.
“Pamoja na msamaha, Debora aliendelea kuomba afidiwe dola elfu kumi na mbili, mimi nikamwambia nimpatie dola elfu sita lakini aligoma na kutaka hiyo hivyo tukashindwa kuafikiana.
VITISHO KWA DIAMOND
“Baada ya kuona tumeshindwa akaanza kututishia kuwa Diamond ni kaka yake hivyo anahusika na msala huo.
“Kweli polisi walifika na kumkamata Diamond, tukawaambia kuwa Rommy Jones si DJ wetu na kwamba tulimkodi tu na tayari ameshaondoka zake kwao.
“Baada ya kuona hivyo hawakuwa na jinsi, wakamwachia Diamond na sisi tukaendelea na shoo zetu.
“Hayo yote yalitokea tukiwa tumebakiza shoo mbili tumalize ziara hiyo hivyo Rommy Jones akawa ‘wanted’ ndiyo maana aliondoka mapema kurejea Tanzania,” alimaliza kusimulia Sallam.
DIAMOND ANASEMAJE?
Alipotafutwa Rommy Jones simu yake haikuwa hewani lakini kwa upande wake Diamond alisema kuwa Sallam ndiye mwenye mkanda mzima hivyo kama alishafafanua ndivyo ilivyokuwa.
-Chanzo: GP

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA