HAYA NDO MANENO YA KWANZA YA MAMA ANNE KILANGO BAADA YA KUTUMBULIWA JIPU NA RAIS MAGUFULI
Leo taarifa ambayo metrend vya kutosha kwa muda mfupi, ni kuhusu Rais
wa J.M wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa
mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mama Anne Kilango Malecela katika nafasi
hiyo.
Mwanasiasa huyu Mkongwe amekumbwa na Panga hili baada ya kutoa
taarifa hadharani kuwa, Mkoa wa Shinyanga haukuwa na watumishi hewa.
Kauli ambayo ilikinzana na tume rasmi ya uchunguzi iliyotumwa mkoani
humo, ambapo iligundua watumishi hewa 45 na bado uchunguzi Zaidi
unaendelea.
Akiongea na kituo cha radio cha Times Fm,Kilango amedai kuwa hana taarifa juu ya utenguzi wa nafasi hiyo kutoka kwa aliyemteua.
“Jamani Mimi sina taarifa sipendi kukizungumzia maana yake sijaambiwa
na aliyeniteua, sina la kukwambia.” Alisema na kukata simu.
Anne Kilango Malecele amedumu kwenye nafasi hiyo kwa majuma kadhaa, hata mwezi mmoja hajafikisha.
Maoni
Chapisha Maoni