CHEZEA LIVERPOOL WEWE? MUULIZE DORTMUND! YATINGA NUSU FAINALI.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Liverpool imefuzu kucheza nusu fainali ya Europa Cup huku ikilazimisha kusawazisha mabao matatu kabla ya kufunga la nne.
Ikiwa
nyumbani, Liverpool ilifungwa mabao 2-0 yaliyodumu hadi mwisho wa
kipindi cha kwanza, kabla ya kuanza kusawazisha katika kipindi cha pili.
Lakini
hata baada ya kupata moja lililofungwa na Divok Origi katika dakika ya
48, Marco Reus akaongeza jingine yaani la tatu kwa Dortmund katika
dakika ya 57.
Baada
ya hapo, Liverpool wakakaa na kuanza kurudisha bao moja baada ya
jingine wakianza na dakika ya 66 kupitia Mbrazili, Phillippe Coutiho
aliyepiga shuti kali kimo cha mbuzi.
Kocha
wa Liverpool, Jurgen Klopp ambaye ni kocha wa zamani wa Dortmund, ndiye
aliyeonekana mwenye furaha zaidi huenda kupita mtu mwingine yoyote.
Beki
Mamadou Sakho akaongeza bao la kichwa katika dakika ya 78 kabla ya beki
mwingine wa kati, Dejan Lovren kumaliza kazi katika dakika ya 90
akipiga kichwa krosi safi ya James Milner aliyeng’ara katika mechi ya
leo.
Liverpool wameonyesha kuwa kweli “U ll Never Walk Alone” kutokana na walivyojituma tokea mwanzo hadi mwisho wa mechi.
Liverpool wanavuka kwa jumla ya mabao 5-4 kwa kuwa katika mechi ya kwanza nchini Ujerumani, walilazimisha sare ya bvao 1-1.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni