AFISA TARAFA WA KIBITI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani Boniventura Mushongi akizungumza na waandishi wa
habari kuhusina na tukio la kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa
Afisa Tarafa wa Kibiti kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la
sita katika shule ya Kitunda.(Picha na Victor Masangu)
NA VICTOR MASANGU, PWANI
JESHI la
polisi Mkoa wa Pwani limemkamata na kumfikisha mahakamani Afisa Tarafa
wa Kibiti Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani Selemani Mpangile almaarufu
babu konyeza kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita
katika shule ya msingi kitunda.
katika shule ya msingi kitunda.
Akizungumza
na Mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Pwani Boniventura Mushogi amesema kwamba tukio hili limetokea juzi
majira ya saa 10 jioni ambapo mtuhumiwa aliamua kutenda kosa hilo
kinyume na sheria na taratibu za nchi.
Mushongi
alisema kwamba jeshi la polisi litaendelea kuvalia njuga vitendo vya
ubakaji kwa watoto wadogo kwani kunaweza kuwasababishia madhara makubwa
watoto hao kutokana na kufanyiwa vitendo kama hivyo wakiwa na umri
mdogo.
Kamanda
Mushongi amefafanua kuwa tukio hilo la ubakaji mtuhumiwa alilifanya
katika ofisi yake wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akipita nje ya jengo
hilo na ndipo alipomwita na kuingia ndani ambapo alimziba mdomo wake kwa
koti leke ili asipige kelele kasha kutekeleza azma yake ya kumbaka .
Katika
hatua nyingene Kamanda ametoa onyo kwa wanafunzi kuachana na tabaia ya
kuwa na tamaa ya kupenda vitu vya bure, na kutoa wito kwa wazazi na
walezi kuhakikisha wanawatunza na kuwalea watoto wao katika misingi
mizuri ya kimaadili na sio kuwa na fikra potofu.
“mimi
napenda kutoa onyo kwa wanafunzi na watoto waache kabisa tabia ya kuwa
na tama, kwani wakifanya hivyo matokeo yake ndio hayo kwani wakati
mwingine wanapenda vitu vya bura kama pipi, soda kwa hivyo hii ni hatari
sana, pia na wazazi wahakikishe wanawalinda watoto wao,” alisema
Mushongi.
MATUKIO
ya vitendo vya ubakaji kwa watoto wadogo katika Mkoa wa Pwani bado
yanaonekana kuwa ni tatizo kubwa hivyo kunahitajika juhudi za makusudi
zifanyike na serikali katika kuwachukulia hatua kali za kisheria na
kutoa adhabu kali kwa wale wote watanaobainika kuhusika katika matukio
kama hayo.(P.T)
Maoni
Chapisha Maoni