RAIS:DKT. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA YA JUU (FLYOVER)
Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi
la ujenzi wa barabara ya juu(Flyover) katika makutano ya TAZARA na ufunguzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Siku
ya Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais ataweka jiwe na
msingi la ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya barabara Nyerere
na Mandela (Flyover ya TAZARA).
Jumanne
tarehe 19 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais atafungua rasmi Daraja la
Kigamboni lenye urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande
wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5. Ujenzi huu
umefanywa na Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni
ya China Bridge Engineering Group.
Aidha
wakati tunasubiri uzinduzi rasmi, Wananchi na magari yenye uzito
usiozidi tani 10 yataruhusiwa kutumia Daraja la Kigamboni kuanzia
Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 ili kuwawezesha kuelewa vizuri
miundombinu na matumizi ya daraja.
Utekelezaji
wa miradi hii ni mojawapo ya jitihada za Serikali za kuboresha
miundomninu na kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es
salaam.
Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
14 Aprili, 2016
Maoni
Chapisha Maoni