Shamsa Ford afurahia kurudiana na Ney wa Mitego

post-feature-image 
Baada ya kauli ya rapa Ney wa Mitego kwa mpenzi wake wa zamani, Shamsa Ford kwamba kama anachagua wasichana wa kurudiana naye atakuwa wa kwanza kutokana na ukarimu na mapenzi yake, mrembo huyo ameibuka na kufurahia kauli hiyo.

Shamsa aliliambia MTANZANIA kwamba, “Mimi na Ney tuliwahi kuwa wapenzi japo tumeachana ila kiukweli tulipendana sana na kama tutarudiana hakuna tatizo kwa kuwa nampenda sana.

Tuliachana na Ney kutokana na maneno maneno ya watu waliokuwa hawapendi penzi letu, lakini kama anataka turudiane nipo tayari,” alijieleza Shamsa huku akifurahia kauli zake hizo.

Aliongeza kuwa yeye si mnafiki kwa alichonacho moyoni na hawezi kuongea kwa kashfa kama baadhi ya waigizaji wenzake wanapotofautiana ama kuachana na waliokuwa wapenzi au waume zao.

Shamsa Ford amewahi kutamba na filamu mbali mbali ikiwepo ‘Bado natafuta’ na ‘Chausiku’.
- Mtanzania

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA