TETESI: Donald Ngoma wa Yanga kucheza Europa msimu ujao?
Ngoma aliye katika msimu wake wa kwanza kwenye Mkataba wa miaka miwili aliosaini kutoka FC Platinums ya Zimbabwe Julai 2015, ametokea kuwa kipenzi cha wana Yanga
Timu moja ya Ligi Kuu ya Yugoslavia ambayo mwakani itacheza michuano ya Europa League inamtaka mshambuliaji wa Yanga SC, Mzimbabawe Donald Dombo Ngoma.
Kwa mujibu wa BinZubeiry Chanzo cha habari kutoka Yanga kimesema kwamba klabu hiyo inataka kufanya mazungumzo na uongozi juu ya a biashara ya Ngoma.
Chanzo hicho kilisema katika barua yao ambayo wameituma tena kuwakumbusha Yanga juu ya kumuhitaji Ngoma, wamesema kwamba wako tayari kumnunua kwa dau la Dola za Marekani 350,000 (zaidi ya Sh. milioni 700 za Tanzania).
"Yule wakala bado anakumbusha barua yake kuhusiana na kumuhitaji Ngoma, lakini Yanga hawataki hata kukaa mezani kuzungumza, na wamesema wako tayari kuongeza dau endapo watatakiwa kufanya hivyo," kilisema chanzo hicho.
Kiliendelea kusema kwamba straika mwenyewe yuko tayari kwenda kujiunga na timu hiyo na anaitaka Yanga ikubali kufanya mazungumzo.
Ngoma aliye katika msimu wake wa kwanza kwenye Mkataba wa miaka miwili aliosaini kutoka FC Platinums ya Zimbabwe Julai 2015, ametokea kuwa kipenzi cha wana Yanga kutokana na kazi yake dimbani.
Maoni
Chapisha Maoni