Serikali yakamata Mzigo wa Maana wa Tanzanite Ukitoroshwa nje

Serikali imefanikiwa kuyakamatwa madini ya Tanzanite yenye thamani ya Sh2.5  bilioni yaliyokuwa njiani kusafirishwa nje ya nchi bila kulipiwa vibali kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana.

Hayo yameelezwa leo jijini hapa na Kaimu Kamishna wa madini nchini, Mhandisi Ally Namaje wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya tatu ya kimataifa ya madini ya Vito yanayofanyika jijini hapa.

Mhandisi Namaje amesema madini hayo yaliyokuwa na uzito wa Kilo  mbili ni sehemu tu ya madini yanayoendelea kutoroshwa na watanzania wasiokuwa wazalendo na nchi yao lakini hata hivyo Serikali inaendelea kuziba mianya yote ya utoroshwaji wa madini hayo nje ya nchi.

"Sheria inasema baada ya madini hayo kukamatwa tunayataifisha na kuyauza kwa mnada, kwa hiyo katika maonyesho haya tutayauza katika mnada wa hadhara ili kila mtu mwenye uwezo aweze kununua," amesema Namaje.

Amesema pia katika kipindi hicho wizara yake imefanikiwa kukamata madini ya Dhahabu yakiwa njiani kutoroshewa nje ya nchi ambayo na yalikuwa njiani kuuzwa kwenye mnada wa hadhara katika maonyesho hayo.

Akizungumzia faida za maonyesho hayo Namaje amesema katika maonyesho ya mwaka jana Serikali ilifanikiwa kupata mapato ya Sh301 milioni  kutokana na mrahaba uliotokana na mauzo ya Tanzanite iliyofikia Sh7.2 bilioni.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 Tanzania imeweza kupata kodi ya tozo kupitia madini ya Tanzanite inayofikia dola za kimarekani  Sh5.4 milioni ikiwa ni wastani wa dola moja milioni kwa mwaka na kwamba fedha hizo zimetokana na uwekezaji wa kampuni ya Tanzanite One.

Maonyesho hayo yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu kwa niaba ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk Merdad Kalemani ambaye aliwataka wafanyabiashara wa madini kufuata sheria za nchi ili kuepuka kufilisiwa endapo watakamatwa wakitorosha madini nje ya nchi.

Chanzo:Mwananchi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA