SHEIKH AFUNGWA JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MWANAFUNZI
Mahakama ya
Wilaya ya Kigoma imemhukumu Sheikh wa Msikiti wa Goma, Hassan Bamba
(48), kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kubaka.
Sheikh
huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa
darasa la sita katika Shule ya Msingi Kitongoni, mwenye umri wa miaka 14
na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.
Hukumu
hiyo ilitolewa jana na Hakimu wa Mahakama hiyo, Frola Mtariania, baada
ya upande wa mashtaka kuthibitisha kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.
Hakimu
Frola, akitoa hukumu hiyo, alisema mahakama inatoa adhabu kali dhidi ya
mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa viongozi wengine wenye tabia ya
kikatili kama yake.
Alisema
upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi watano, pamoja na kielelezo cha
PF3, ambacho kilithibitisha kwamba Sheikh Bamba mshtakiwa alitenda kosa
hilo.
Alipotakiwa
kujitetea ili kupunguziwa adhabu, akiongozwa na wakili wa kujitegemea
Method Kabuguzi, mshtakiwa aliangua kilio na kuiomba mahakama impunguzie
adhabu kwa sababu ana familia inamtegemea.
Pia alidai ni kosa lake la kwanza tena shetani alimwingilia. Hakimu Frola alitupilia mbali utetezi huo na kusema:
"Mshtakiwa
ukiwa kiongozi wa dini, kitendo ulichokifanya si cha kijamii maana wewe
ndiwe unayefundisha watu kuachana na maovu cha kushangaza unakuwa ndiye
wa kwanza kuyatenda maovu.
"Sasa
utakwenda gerezani miaka 30 ili ukajifunze tabia ya kuwa kiongozi bora
wa dini, kwa sababu huku uraiani umeshindwa kuishi na jamii."
Awali,
akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Anita Julius, alidai kuwa
Januari Mosi, mwaka huu, saa 4 asubuhi eneo la Ujiji Kigoma, mshtakiwa
huyo alibaka msichana huyo.
Ilidaikwa
kuwa siku ya tukio mtoto aliyebakwa akiwa na pacha wake, ambao baba yao
ni rafiki wa sheikh huyo, walikwenda kwa sheikh huyo kwa ajili ya
kuombewa duwa na kufanyiwa dawa kwa ajili ya kufaulu mtihani wa kuingia
darasa la saba.
Kwa
mujibu wa hati ya mashtaka, baada ya kufika, Bamba alimtuma mwenzake
aende shuleni kuchukua mchanga na ndipo alipomfanyika kitendo hicho yule
aliyebaki.
Mwenzake aliporejea, ilidaiwa kuwa alimkuta pacha wake analia na alipomuuliza alimjibu kuwa amebakwa na Bamba.
Umati
mkubwa wa wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, wakiwamo waumini wa
msikiti aliokuwa akiswalisha, ulikusanyika mahakamani na kushuhudia
Sheikh huyo anapelekwa jela
Maoni
Chapisha Maoni