ANNA TIBAIJUKA ATAKIWA KULIPA TSH MILIONI 586 KAMA KODI YA PESA ZA ESCROW ALIZO BEBA
Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema yupo
tayari kulipa kodi ya mapato ya Sh586 milioni iwapo Mahakama itaamuru
hivyo.
Kodi hiyo inatokana na Sh1.617 bilioni alizopewa na mfanyabiashara maarufu nchini, James Rugemalira ambazo zilidaiwa kuchotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Profesa Tibaijuka aliyasema hayo jana baada ya taarifa kwamba Bodi ya Rufani ya Kodi Tanzania (TRAB), imeagiza utekelezaji wa suala hilo ili kutimiza matakwa ya sheria kuhusu mapato nchini.
Mbunge huyo alifafanua kuwa, anatambua kulipa kodi ni suala la kila mwananchi na anachotaka ni ufafanuzi wa uhusiano uliopo kati ya mapato na kodi.
Alisema lengo ni kutaka kujua iwapo mchango ni sehemu ya fedha zinazostahili kutozwa kodi, bila kujali zimepokelewa zikiwa taslimu au kupitia kwenye akaunti benki.
Msemaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo alithibitisha kutolewa kwa hukumu hiyo kwenye pingamizi la makadirio aliloliweka mbunge huyo na kueleza kuwa bado anaweza akatafuta haki kwenye mamlaka za juu kama hajaridhika.
Mbunge huyo wa Muleba Kusini, alitakiwa kulipa fedha hizo baada ya TRAB kutupilia mbali rufaa yake ya kupinga kulipa zaidi ya Sh500 milioni.
Profesa Tibaijuka, Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alikata rufaa hiyo baada ya TRA kumtaka alipe kodi ya mapato Sh586,364,625 kutokana na fedha alizopokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, Rugemalira.
Profesa Tibaijuka ambaye alipokea fedha hizo kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya Mkombozi, zilisababisha kuvuliwa uwaziri na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
Alisema fedha hizo hazikuwa zake binafsi bali zilitolewa msaada kwa Taasisi ya Joha Trust.
Hata hivyo, TRA kupitia kwa Wakili wake, Noah Tito ilisema Tibaijuka anawajibika kulipa kodi hiyo kwani fedha hizo ziliingia katika akaunti yake binafsi

“Ni kweli ninadaiwa kodi ya Sh586 milioni, ila nimeenda mahakamani kutaka ufafanuzi kama ni halali kufanya hivyo kwa fedha zilizotokana na mchango,” alisema Profesa Tibaijuka na kuongeza “Nilipewa fedha kwa ajili ya shule lakini nadaiwa kama ni kipato binafsi, hivyo nataka Mahakama iseme, ikikubali nitalipa bila shida yoyote.”
Mbunge huyo alifafanua kuwa, anatambua kulipa kodi ni suala la kila mwananchi na anachotaka ni ufafanuzi wa uhusiano uliopo kati ya mapato na kodi.
Alisema lengo ni kutaka kujua iwapo mchango ni sehemu ya fedha zinazostahili kutozwa kodi, bila kujali zimepokelewa zikiwa taslimu au kupitia kwenye akaunti benki.
“Nipo msibani hivi sasa. Watu wanakuja kunipa pole, wengine wanatoka Dar na wasioweza wanatuma michango yao na hapa ndipo nisipoelewa dhana ya kodi kwenye michango. Hii nayo inastahili kuingizwa kwenye mkumbo huo?” alihoji.
Msemaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo alithibitisha kutolewa kwa hukumu hiyo kwenye pingamizi la makadirio aliloliweka mbunge huyo na kueleza kuwa bado anaweza akatafuta haki kwenye mamlaka za juu kama hajaridhika.
“Shauri lake liliamriwa Machi 29 na akatakiwa kulipa kiwango hicho alichokadiriwa,” alisema.
Mbunge huyo wa Muleba Kusini, alitakiwa kulipa fedha hizo baada ya TRAB kutupilia mbali rufaa yake ya kupinga kulipa zaidi ya Sh500 milioni.
Profesa Tibaijuka, Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alikata rufaa hiyo baada ya TRA kumtaka alipe kodi ya mapato Sh586,364,625 kutokana na fedha alizopokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, Rugemalira.
Profesa Tibaijuka ambaye alipokea fedha hizo kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya Mkombozi, zilisababisha kuvuliwa uwaziri na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
Alisema fedha hizo hazikuwa zake binafsi bali zilitolewa msaada kwa Taasisi ya Joha Trust.
Hata hivyo, TRA kupitia kwa Wakili wake, Noah Tito ilisema Tibaijuka anawajibika kulipa kodi hiyo kwani fedha hizo ziliingia katika akaunti yake binafsi
Maoni
Chapisha Maoni