Video: Rais Magufuli Awajibu Haki za Binadamu, Asema Nao Wanaweza Kuwa Majipu Kwa Kutetea Maovu....
Katika hali inayoonyesha kuwa na majibizano kati ya Rais Magufuli na
Kituo Cha Haki za Binadamu LHRC kinachoongozwa na Dr. Hellen Kijo
Bisimba, leo Rais Magufuli hadharani kasema wanaosema amekiuka haki za
binadamu kumsimamisha ndugu Kabwe hadharani walitakiwa pia waseme vivyo
hivyo kipindi anamuapisha hadharani kwa kuwa ni mteule wake, Amesema hao
Waliotumbuliwa wamewaibia Watanzania hadharani hivyo inabidi
watumbuliwe hadharani nao wapate maumivu kama waliyoyapata
Watanzania...Hivyo, ni vyema wakaiacha serikali ikafanya kazi yake, na
ikiwezekana itabidi awachunguze hao LHRC credibility yao kama wanatetea
mambo maovu inawezekana nao ni majipu..
Maoni
Chapisha Maoni