TATOO YA WEMA, DIAMOND KWA WAZAZI WAO
Tofauti na mastaa wengine ambao huandika majina ya wapenzi wao kwenye
miili yao kuonesha jinsi wanalivyo na mapenzi nao, Nasibu Abdul
‘Diamond’ na Wema Sepetu wamekuwa tofauti, Ijumaa limegundua.
Tattoo ya Diamond Platinum ikionekana kwenye mkono wake wa kushoto.
Mastaa hawa wameonyesha kuwa na mapenzi na wazazi wao ambapo
mwandishi wetu amebaini Diamond ameandika jina la mama yake mkononi huku
Wema akiandika jina la baba yake mkononi pia.
Wote wamefanya hivyo kwenye mikono yao ya
kushoto sambamba na uwepo wa tatoo nyingine ambapo Wema ameandika ‘Daddy
Sepetu’ na Diamond akaandika Sandra…’
Tattoo ya Wema Sepetu ikionekana kwenye mkono wake wa kushoto.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wao wamedai huenda penzi la mastaa
hao si la kudumu ndiyo maana wamekwepa kuandikana ili isije ikawa shida
pale watakapomwagana.
Maoni
Chapisha Maoni