JACQUELINE WOLPER AFYATA MKIA...AMWANGUKIA YULE PEDESHEE WA KIKONGO!
Staa
wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe. Kikizungumza na Risasi
Mchanganyiko, chanzo makini kilidai kwamba baada ya gazeti ndugu na hili
kuripoti habari ya Wolper kumchana Mkongo huyo huku akidai hana hadhi
ya kuwa naye, wiki iliyopita alionekana kwenye Hoteli ya Double
Treeiliyopo Masaki jijini Dar ambako ndipo alipofikia mwanaume huyo.
Kiliendelea kueleza kwamba mwanadada huyo alifika hotelini hapo kwa
ajili ya kumuomba msamaha Mkongo na alikuwa akifanya jitihada kubwa ili
asamehewe kwa kumtumia mwanamuziki wa FM Academia, raia wa Kongo, Patcho
Mwamba amuombee msamaha.
BAADA
ya hivi karibuni kumchana laivu Mkurugenzi wa Mwami Foundation, raia wa
Kongo, Mwami Rajabu, staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe
anadaiwa kumwangukia jamaa huyo na kumuomba msamaha.
“Nimemuona Wolper akiwa na huyo Mkongo kwenye hoteli hiyo aliyofikia ambapo kilichompeleka ni kuomba msamaha kutokana na maneno aliyozungumza kwenye gazeti,” kilisema chanzo hicho
Maoni
Chapisha Maoni