HOFU YATANDA,MSHITUKO WA VIFO VYA WASANII... NDANI YA MASAA 24 WAFARIKI DUNIA WANNE

Misiba kila kona! Achilia mbali watu wasiokuwa na majina hasa vijana wadogo, ndani ya saa 24 wamefariki dunia wasanii wanne wa kutoka kwenye tasnia za Bongo Movies na Bongo Fleva, Amani lina habari yenye kuumiza moyo.




Benson Okumu, enzi za uhai wake akiwa na mtoto wa marehemu George Okumu Otieno ‘Tyson’ , Sonia.
HAWA HAPA
Matukio hayo yalitokea kati ya Jumatatu jioni na Jumanne asubuhi ambapo kutoka kwenye tasnia ya filamu waliotangulia mbele ya haki ni pamoja na Sherry Salum ‘Sheri Magali’, Arafa na Benson Okumu Otieno.

Kwa upande wa Bongo Fleva, Yessaya Ambikile ‘YP’, naye alitangulia mbele ya haki ikiwa ni siku chache tu alionekana kwenye kumbi mbalimbali jijini Dar. 
ALIANZA MDOGO TYSON
Jumanne jioni, gazeti hili lilipokea kwa masikitiko kifo cha mdogo wa marehemu George Okumu Otieno ‘Tyson’ aitwaye Benson Okumu Otieno ‘Benii’ ambaye alifariki dunia baada ya kupata homa kali na kuchanganyikiwa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA