LADY JAYDEE AVUNJA MKATABA NA GARDNER!
HABARI
mpya kutoka kwa mastaa wanaodaiwa kuvunjika kwa ndoa yao, Judith
Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’, inasemekana
wamevunja mkataba wa kuendesha Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Ada
Estate, Kinondoni jijini Dar.
Mbongo
Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’. Kwa mujibu wa mtoa habari
wetu, wawili hao walidaiwa kufikia uamuzi wa kuvunja mkataba baada ya
kuona ndoa yao inasuasua kutokana na migogoro.“Lady Jaydee au Jide
alipoona mambo yanakwenda ndivyosivyo alimshauri Gardner wavunje
mkataba
wa Nyumbani Lounge ili kila mmoja awe na businesses (biashara) zake.
“Walimfuata mmiliki wa jengo, wakamwambia kwamba wanavunja,
akawakubalia,” kilinyetisha chanzo makini. Chanzo hicho kilizidi kwenda
mbali zaidi na kudai kuwa mgahawa huo kwa sasa unamilikiwa na mzungu.
Maoni
Chapisha Maoni