DUNIA INA MAMBO: DAWA YA KUKAMATA WEZI YAZUA BALAA...WAHUSIKA WAPAGAWA NA KUANZA KULA NYASI!
Watu
saba kati ya 100 Kijiji cha Kenyamanyori, Kata ya Turwa, Wilaya ya
Tarime walioshiriki kunywa dawa ya mganga wa kienyeji aliyeletwa kutoka
Busia nchini Kenya wameingia kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa
kutimiza masharti ya kulipa Sh3 milioni kila mmojaWanakijiji hao
walikusanyika juzi asubuhi baada ya kengele ya kijiji kugongwa na
uongozi, huku wakieleza kwamba ilikuwa siku ya nne kwa kengele hiyo
kugongwa lengo
likiwa ni kuzungumzia wizi unaoendeshwa na watu wasiojulikana.Inadaiwa wizi wa kuvunja maduka umekithiri kijijini hapo, baada ya wanakijiji hao kuwasili eneo la mikutano, walielezwa kusudio la kengele kuwa ilikuwa ni kutokana na kukithiri kwa matukio ya uhalifu.

Miongoni
mwa waliovunjiwa duka ni Ayubu Wambura, anayedaiwa kuleta mganga kutoka
Busia nchini Kenya kuwabaini wahusika, hivyo kila mmoja aliombwa kunywa
dawa ya mganga huyo au kuacha maana ni hiyari.
Maoni
Chapisha Maoni