MAKUBWA NA MAZITO HAYA: BMW LA WEMA UTATA MTUPU, MKASA MZIMA UPO HAPA!
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akiwa ndani ya Gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa na meneja wake.
Achana
na lile gari aina ya Nissan Murano alilozawadiwa na mwandani wake,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, gari lingine aina ya BMW 545i
aliloletewa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kwenye pati ya
‘bethidei’ yake ni utata mtupu na maswali kibao.
Katika
shughuli hiyo, waalikwa ambao sehemu kubwa walikuwa watu wenye majina,
walikula na kunywa kuanzia mchana hadi usiku mnene.
Akiwa
Marekani, Diamond alimuagiza mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ apeleke
gari aina ya Nissan Morano lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 36 za
madafu ikiwa ni zawadi ya jamaa huyo kwa mkewe huyo mtarajiwa.
Gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na meneja wake.
Alipoliona gari hilo, Wema alipigwa na butwaa huku akimshukuru Diamond ambaye kwa sasa amempachika jina la Chibu baada ya lile la Dangote ‘kueksipaya’.
Maoni
Chapisha Maoni