KAJALA, WEMA SEPETU WATOANA JASHO POLISI.
Mwigizaji Kajala Masanja
Kufuatia
matusi ya mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam
Sepetu kwenda kwa mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, mastaa hao wamejikuta
wakitoana jasho kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama almaarufu
Mabatini jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita.Duru za ‘kiubuyu’
zilidai kwamba Kajala, baada ya kuchoshwa na matusi hayo ambayo
yalianzia kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Wema, alijikuta akiishiwa na
uzalendo kisha kuingia mzigoni ili kukomesha matusi hayo kwenye mitandao
ya kijamii.
Ilidaiwa
kwamba, Kajala akiwa na timu yake (Team Kajala) alifanikiwa kumtia
mbaroni dada mmoja aliyetajwa kwa jina la Matrida akidaiwa kwamba ni
mfuasi wa Wema (Team Wema).
Ilisemekana
kwamba Matrida anayetumia jina la ‘Mat Kiboko Yao’ kwenye ukurasa wake
wa Instagram ndiye ambaye amekuwa akiongoza jahazi la kumtusi Kay.
Ilizidi
kunyunyizwa kwamba sakata hilo la kuanikwa Instagram lilianza siku mbili
baada ya ile pati ya kuzaliwa ya Wema ambapo Mat Kiboko Yao alimtukana
Kajala matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini) kupitia ukurasa wake
kwenye mtandao huo.
Ilidaiwa
kwamba Kajala alipoona amechoka kutukanwa, alitafuta wataalam ili kujua
namna ya kumkamata na alipomjua ndipo akakimbilia Kituo cha Polisi cha
Mabatini kwenda kutoa taarifa.
RB
Staa
wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu.Gazeti hili lilifanikiwa kunasa
namba ya jalada la kesi hiyo iliyosomekaKJN/RB/8854/2014-MATUMIZI YA
MATUSI MTANDAONI.
Ilisemekana
polisi walitumia mbinu zao na kufanikiwa kumkamata Mat Kiboko Yao na
kumweka nyuma ya nondo za mahabusu kituoni hapo ndipo sarakasi za pande
mbili zikaanza.
KWANZA
Mara tu
baada ya Mat Kiboko Yao kukamatwa mishale ya saa 2:00 usiku, taarifa
zilisambaa kama moto wa kifuu ndipo Team Wema ikaingia mzigoni kutaka
kumtoa mwanadada huyo lakini wakagonga mwamba.
WEMA, PETIT MAN WATINGA MABATINI
Ilidaiwa
kwamba, baada ya Mat Kiboko Yao kutiwa mbaroni, Wema na jeshi lake
akiwemo Petit Man walitinga Mabatini kwa ajili ya kumtoa mwanadada huyo
lakini aligonga mwamba na kumuacha akilala kituoni hapo.
“Yaani
ulikuwa ni usiku wa kutoana jasho na kupimana ubavu kwamba nani ni nani.
Ilikuwa akitoka Kajala kuhakikisha kwamba mtuhumiwa wake aachiwi, Wema
naye anatinga kituoni kwa mbwembwe kutaka Mat Kiboko Yao aachiwe kwa
gharama yoyote.
“Hapo
ndiyo ngoma ilikuwa nzito, kila mmoja alikuwa anamuonyesha mwenzake kuwa
ni zaidi na ni maji marefu hadi kulipokucha muvi likaendelea,” alisema
shuhuda aliyefuatilia sakata hilo kinagaubaga.
Mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu.WAANDISHI WAPEWA UBUYU, WATINGA MABATINI
Kulipokucha, waandishi wetu walipewa ubuyu huo ndipo wakatinga Mabatini kisha wakatega ‘rada’ zao na kuweka doria.
Wanahabari wetu, wakiwa kituoni hapo walimshuhudia Kajala akilinda kituoni hapo asitokee mtu yeyote akamtoa Mat Kiboko Yao.
Hata
hivyo, alipoulizwa Kay kulikoni kuwa eneo hilo alisema alikuwa ameitwa
kwa ajili ya kusuluhishwa badala ya kupoteza muda kwa jambo kama hilo.
KAJALA NA KUNDI LAKE
Awali Kay
alionekana akiingia kituoni hapo na kundi lake la watu watatu akiwemo
mwanaume mmoja ambapo yeye aliingia mpaka kwenye chumba cha mkuu wa
kituo.
Kajala
akiwa kwa mkuu wa kituo, haikujulikana kilichokuwa kikiendelea ndani
kwani kulikuwa na kikao cha muda mrefu ambapo ghafla Kajala na mtuhumiwa
wake waliyeyuka.
WEMA AINGIA MITINI
Wakati
hayo yakiendelea kituoni hapo, si Wema wala jeshi lake waliofika kwa
ajili ya kumtetea Mat Kiboko Yao ambaye ndiye kiongozi wa Timu Wema kwa
kutukana.
Hata hivyo, baadaye alionekana mmoja wa marafiki wa karibu ambaye ni ndugu wa Mat Kiboko Yao aliyekuwa akihaha kumtoa mwenzake.
TUJIKUMBUSHE
Hivi
karibuni Mama Wema alimtolea uvivu Kajala na kumtusi ndipo akafufua upya
kile kidonda cha Sh. milioni 13 ambazo Wema alimlipia Kay asiende jela
na kinachoonekana, bado fedha hizo ni tatizo kubwa.
Maoni
Chapisha Maoni