HATIMAYE MH. MBOWE ATOLEA UFAFANUZI WA PICHA YAKE YA KIMAHABA ILIYOSAMBAA MITANDAONI!
Week
iliyopita Picha hiyo hapo juu ilienea mitandaoni ukimuonesha Freeman
Mbowe na Mkewe Wakibusiana Live ....Mbowe Ameongea haya Kuhusu Picha
hiyo :
“Kwanza
mke wangu alikuwa anatimiza umri wa miaka 50 ya kuzaliwa, vilevile
firstborn wetu Dudley alikuwa amemaliza shahada yake ya kwanza Chuo
Kikuu cha Sussex, Uingereza, kwa mambo hayo mawili, tuliona ipo haja ya
kufanya sherehe, ukizingatia watoto wetu wengine wawili Nicole na Denis
walikuwa wamerejea nchini kwa sababu nao wanasoma nje ya nchi.
“Siku hiyo ya tukio ilikuwa Jumapili, tulianza kwa kwenda kanisani
Azania Front tukatoa sadaka, baada ya hapo tulikwenda Serena Hotel
kwenye Ukumbi wa Kivukoni ambako chakula cha mchana kilikuwa
kimeandaliwa, tukajumuika na ndugu wengine pamoja na marafiki.
“Haikuwa sherehe tu kusema labda nilikurupuka kumbusu mke wangu,
ilikuwa sherehe ya kifamilia, kumpongeza mke wangu na mtoto wetu,”
alisema Mbowe.
Maoni
Chapisha Maoni