Cloud Afunguka Baada Ya Tuhuma za Kumfanyia Fitina Frank Mwikongi Deal La Uingereza.
Cloud |
Msanii mkongwe wa filamu Tanzania Issa Musa ‘Cloud’ amekana tuhuma
zinazosambazwa mtandaoni kuwa alimfitini muigizaji mwenzake, Mohammed
Mwikongi ‘Frank’ ili kumzuia asisafiri kuelekea Uingereza miezi michache
iliyopo.
“Mimi sikumfitini Frank, yule mtu
alinifuata mwenyewe kwa makubaliano ya mdomo kuwa nikacheze filamu,
sikuwa peke yangu, tuliongozana na kina Monalisa na Riyama, tatizo ni la
huyo aliyenipeleka kule, nilifanya mambo kwa mazoea na ndiyo sababu
anaamua kusambaza uongo dhidi yangu,” alisema Cloud wakati akizungumza
na Globalpublishers
Cloud aliwasihi wasanii wenzake nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea
bali wahakikishe wanaingia mikataba ya maandishi ili wawe na ushahidi
wakati waliokubaliana nao kazi wanapoleta ujanjaujanja kama ilivyomtokea
yeye katika safari hiyo ya Uingereza ambayo sasa inamletea uadui na
Frank.
Frank
Maoni
Chapisha Maoni